Loading the player...


INFO:
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, amewasili mkoani Iringa na kupokelewa na Viongozi Mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba, katika Uwanja wa Ndege (Iringa Airport). Dkt. Biteko amewasili Mkoani Iringa April 26, 2025 ambapo anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ibada na Sherehe za kuwekwa wakfu Askofu Mteule Romanus Elamu Mihali kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Kitume la Iringa. Ibada na Sherehe za kuwekwa Wakfu Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa itafanyika Jumapili ya April 27, 2025 Kanisa Katoliki Jimbo la Iringa.